Kamusi ya Tech, toleo 01: maneno 8 ambayo lecturer hakueleza By Privatus Cosmas 2026-10-13 https://depriver.tech/blog/kamusi-ya-tech/ API, bug, Git, deploy, server, cloud, database and framework, explained in plain Swahili with daily-life examples. The first episode of Kamusi ya Tech. Darasani tunasikia maneno haya kila siku, lakini mara nyingi hakuna anayeyaeleza kwa lugha rahisi. Hii ni **Kamusi ya Tech**: maneno ya tech kwa Kiswahili rahisi, kila moja na mfano wa maisha ya kila siku. Toleo la kwanza lina maneno manane. ## API *(nomino)*: Application Programming Interface **Maana:** Njia ambayo programu moja huongea na programu nyingine na kubadilishana taarifa. **Mfano:** Mhudumu wa mgahawa. Unaagiza chakula (request), jikoni wanapika, mhudumu anakuletea (response). Huoni jikoni, unapata chakula tu. *"App yetu inachukua hali ya hewa ya Mbeya kupitia API."* ## Bug *(nomino)* **Maana:** Hitilafu kwenye code inayofanya programu ifanye kitu ambacho hukutarajia. **Mfano:** Calculator inasema 2 + 2 = 22. Kutafuta na kurekebisha bug ndiyo *debugging*. ## Git *(nomino)* **Maana:** Mfumo unaohifadhi historia ya kila mabadiliko kwenye code yako, hatua kwa hatua. **Mfano:** Kama save points kwenye game. Hakuna tena `final_FINAL2.zip`. GitHub ni mahali project za Git zinakaa mtandaoni. ## Deploy *(kitenzi)* **Maana:** Kuhamisha programu yako kutoka kwenye kompyuta yako na kuiweka mtandaoni ili watu waitumie. **Mfano:** Kupika nyumbani dhidi ya kufungua mgahawa. "Inafanya kazi kwenye laptop yangu" haitoshi mpaka u-deploy. ## Server *(nomino)* **Maana:** Kompyuta inayohudumia tovuti au programu kwa watumiaji wengi, masaa 24. **Mfano:** Kama duka lisilofungwa kamwe: wateja (browsers) wanakuja wakati wowote, na duka linawahudumia. ## Cloud *(nomino)*: wingu **Maana:** Kutumia server na huduma za kampuni nyingine kupitia internet badala ya kununua zako. **Mfano:** Kupanga nyumba badala ya kujenga. Google Drive ni cloud: picha zako ziko kwenye server za mtu mwingine. ## Database *(nomino)*: hifadhidata **Maana:** Mahali data huhifadhiwa kwa mpangilio ili itafutwe, ibadilishwe na ipatikane haraka. **Mfano:** Daftari la mauzo la duka, ila unaweza kutafuta mauzo ya mwaka mzima kwa sekunde moja. ## Framework *(nomino)*: kiunzi **Maana:** Msingi uliotengenezwa tayari, wenye sheria na zana, unaojengea programu haraka. **Mfano:** Kiunzi cha nyumba kilichosimamishwa tayari: wewe unajenga kuta na kupamba, hauanzi kuchimba msingi. Mifano: Laravel, React, Django. **Neno gani litoke toleo 02?** Niambie kwenye comments, na share na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza. Slide captions 1. Kamusi ya Tech, toleo 01: maneno 8 ambayo lecturer hakueleza. 2. API: njia ambayo programu moja huongea na programu nyingine. Mfano: mhudumu wa mgahawa. 3. Bug: hitilafu kwenye code inayofanya programu ifanye kitu usichotarajia. 4. Git: mfumo unaohifadhi historia ya kila mabadiliko kwenye code yako. Kama save points kwenye game. 5. Deploy: kuweka programu yako mtandaoni ili watu waitumie. Kupika nyumbani dhidi ya kufungua mgahawa. 6. Server: kompyuta inayohudumia tovuti au programu masaa 24. Kama duka lisilofungwa. 7. Cloud: kutumia server za kampuni nyingine kupitia internet. Kupanga nyumba badala ya kujenga. 8. Database: mahali data huhifadhiwa kwa mpangilio. Daftari la mauzo linalotafutika kwa sekunde. 9. Framework: kiunzi kilichotengenezwa tayari unachojengea programu, kama Laravel, React au Django. 10. Neno gani litoke toleo 02? Niambie kwenye comments.