API, bug, Git, deploy, server, cloud, database and framework, explained in plain Swahili with daily-life examples. The first episode of Kamusi ya Tech.
↓ Download all 10 slides (ZIP)↓ Download article (TXT)All slide images and the full article in one ZIP, ready to save and read offline.
Darasani tunasikia maneno haya kila siku, lakini mara nyingi hakuna anayeyaeleza kwa lugha rahisi. Hii ni Kamusi ya Tech: maneno ya tech kwa Kiswahili rahisi, kila moja na mfano wa maisha ya kila siku. Toleo la kwanza lina maneno manane.
API (nomino): Application Programming Interface
Maana: Njia ambayo programu moja huongea na programu nyingine na kubadilishana taarifa.
Mfano: Mhudumu wa mgahawa. Unaagiza chakula (request), jikoni wanapika, mhudumu anakuletea (response). Huoni jikoni, unapata chakula tu.
“App yetu inachukua hali ya hewa ya Mbeya kupitia API.”
Bug (nomino)
Maana: Hitilafu kwenye code inayofanya programu ifanye kitu ambacho hukutarajia.
Mfano: Calculator inasema 2 + 2 = 22. Kutafuta na kurekebisha bug ndiyo debugging.
Git (nomino)
Maana: Mfumo unaohifadhi historia ya kila mabadiliko kwenye code yako, hatua kwa hatua.
Mfano: Kama save points kwenye game. Hakuna tena final_FINAL2.zip. GitHub ni mahali project za Git zinakaa mtandaoni.
Deploy (kitenzi)
Maana: Kuhamisha programu yako kutoka kwenye kompyuta yako na kuiweka mtandaoni ili watu waitumie.
Mfano: Kupika nyumbani dhidi ya kufungua mgahawa. “Inafanya kazi kwenye laptop yangu” haitoshi mpaka u-deploy.
Server (nomino)
Maana: Kompyuta inayohudumia tovuti au programu kwa watumiaji wengi, masaa 24.
Mfano: Kama duka lisilofungwa kamwe: wateja (browsers) wanakuja wakati wowote, na duka linawahudumia.
Cloud (nomino): wingu
Maana: Kutumia server na huduma za kampuni nyingine kupitia internet badala ya kununua zako.
Mfano: Kupanga nyumba badala ya kujenga. Google Drive ni cloud: picha zako ziko kwenye server za mtu mwingine.
Database (nomino): hifadhidata
Maana: Mahali data huhifadhiwa kwa mpangilio ili itafutwe, ibadilishwe na ipatikane haraka.
Mfano: Daftari la mauzo la duka, ila unaweza kutafuta mauzo ya mwaka mzima kwa sekunde moja.
Framework (nomino): kiunzi
Maana: Msingi uliotengenezwa tayari, wenye sheria na zana, unaojengea programu haraka.
Mfano: Kiunzi cha nyumba kilichosimamishwa tayari: wewe unajenga kuta na kupamba, hauanzi kuchimba msingi. Mifano: Laravel, React, Django.
Neno gani litoke toleo 02? Niambie kwenye comments, na share na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza.